Habari njema kwa wazazi na wanafunzi kuhusu mbinu mpya ya kuchagua shule

- Wazazi na wanafunzi wamepokea habari njema kuhusiana na masomo ya humo nchini

- Kwa mara ya kwanza Wakenya sasa wataweza kujichagulia shule za chekechea na za upili wanazopenda bila tashwishwi

Mambo yamerahisishwa kwa wazazi na wanafunzi baada ya muungano wa shule za kibinafsi ( KPSA) kuzindua njia mpya ya kuchagua shule.

Habari Nyingine: Nyoka avuruga mkutano wa Rais Uhuru Kisumu

Habari Nyingine: Wamkumbuka BAHA wa kipindi cha Citizen TV cha Machachari? Huyu hapa na MPENZI wake (picha)

Mbinu hiyo maarufu kama Somanet inawawezesha wanafunzi kuchagua shule wanazopenda bila tashwishwi yeyote.

Mbinu hii inanuia kuwasaidia wazazi kupata shule kwa haraka punde matokeo ya mitihani hasa ya kitaifa yanapotangazwa.

Habari Nyingine: Jamaa wa MERU ashangaza Wakenya kwa mtindo wake wa nywele (picha)

Wanafunzi wataweza kujua kiwango cha karo inayopaswa kulipwa, historia ya shule, na kila kitu kinachohusiana na shule hiyo kupitia Somanet.

Punde tu mwanafunzi anapochagua shule kupitia Somanet, atapokea maelezo kamili kuhusiana na shule hiyo kupitia barua pepe ama ujumbe mfupi kwa simu.

Pakua APP mpya ya TUKO upate habari BURE!

Mbinu hiyo inatarajiwa kutumika kwa shule za chekechea, za msingi na za sekondari za kibinafsi.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: aron.mtunji@tuko.co.ke

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaIR3f49mn5qakae2brrJnqSaZZusrm7DwLOYs6Fdo65uw8CnmJ%2Btnq%2B2brfUoaysrV2ir6q61GakqbGRYsaiecqumqGZl6qubr%2FHrqOeZpipuq0%3D